Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha


NA WAMJW, DAR ES SALAAM
WAKAZI wa Dar es Salaam wapatao Milioni 4.3 wanatarajiwa kumeza Kingatiba dhidi ya magonjwa ya matende na mabusha (Ngirimaji) pamoja na minyoo ya tumbo, kuanzia Disemba 15 hadi 20, mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD), Dkt. Upendo Mwingira wakati wa Warsha ya Wanahabari kuhusu magonjwa hayo hapa nchini.
Dkt. Upendo Mwingira amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo kwani kingatiba hiyo itatolewa bila malipo katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam.“Hii sio chanjo. Ni kijngatiba na zoezi hili linaenda kumkinga mtu dhidi ya magonjwa ya mabusha na matende pamoja na minyoo na itatolewa kuanzia umri wa miaka 5 na kuendelea” Amasema Dkt.Upendo Mwingira.
Ameongeza kuwa, “Wananchi watakaojitokeza watamezeshwa kingatiba hizo papohapo na zoezi hili utolewa kila mwaka mara moja” amebainisha.Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni pamoja na Usubi,Vikope (Trakoma), ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More