Wanandoa wakabidhiwa jukumu la kusoma taarifa ya habari kwenye luninga wakiwa pamoja - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wanandoa wakabidhiwa jukumu la kusoma taarifa ya habari kwenye luninga wakiwa pamoja

Chombo cha habari cha Citizen nchini Kenya kimewatangaza wanandoa maarufu, Rashid Abdalla na mkewe Lulu Hassan kuanza kusoma taarifa ya habari wakiwa pamoja kila ifikao siku ya Jumamosi na Jumapili.Rashid ambaye ni mume wa mwana dada Lulu alikuwa mtangazaji wa kituo cha NTV kabla ya kujiunga na Citizen ambapo amekabidhiwa majukumu hayo mapya akiwa sanjari na mkewe kwenye kipindi cha Nipashe Wikendi kinachoruka hewani kila Jumamosi na Jumapili kuanzia tarehe 21 mwezi Julai 2018.Kwa mara ya kwanza habari nchini Kenya zitaletwa kwako na mume na mkewe; Rashid Abdalla na Lulu Hassan. Jiunge nao pamoja na Bi Msafwari kila Ijumaa hadi Jumapili kwenye #Nipashe pic.twitter.com/nMG2mhXv6m


— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) July 21, 2018Tukio hili la wanandoa kusoma habari wakiwa pamoja ni kwa mara ya kwanza linatokea nchini Kenya. Rashid Abdalla anachukua nafasi ya Kanze Dena ambaye aliajiriwa na Ikulu ya rais kuwa msemaji mnamo mwezi Juni.


Wakenya wengi wakisubiri kuona ikiwa wapen... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More