'WANAUME KUOGOPA KUPIMA TEZI DUME KISA AIBU NI UJINGA' HAYA YABAINIKA UZINDUZI WA KLINIKI ZA JIONI BUGANDO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

'WANAUME KUOGOPA KUPIMA TEZI DUME KISA AIBU NI UJINGA' HAYA YABAINIKA UZINDUZI WA KLINIKI ZA JIONI BUGANDO


NA. GSENGOtV
Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku, Kushindwa kuzuia mkojo, yaani ukichelewa kidogo unaweza kukutoka bila breki, Maumivu wakati wa kukojoa, Kuishiwa nguvu za kiume, Kupungua kwa uwingi wa mbegu (low sperm count), Maumivu wakati unafika kileleni, Damu kutokea kwenye mkojo au kwenye mbegu za kiume, Maumivu nyuma ya mgongo au hata nyonga nk basi uonapo dalili hizo unaweza kuanza kuhisi una saratani ya tezi dume.
Kupitia dalili hizo ni wazi kwamba afya ya mgonjwa itakuwa matatani kwenye mataabiko.Wahenga walironga mficha maradhi kifo humuumbua. Kila kiungo cha mwanadamu kikipata tatizo ni jukumu la matabibu kufanya uchunguzi na kutoa huduma kwa eneo lililodhurika, Haiingii akilini kwamba uendelee kuteseka ile hali tiba ipo. Nao wataalamu wanasema uchunguzi wa kutumia kidole hauhitaji gharama kubwa kama ilivyo njia nyingine za kutumia vifaa maalum vya uchunguzi.
Ni tamaduni tu za watu wenye mawazo machafu ndizo zinazo wafanya wengi kudhani kipimo cha kidole ni udhalilisha... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More