WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA


Wanawake washiriki kujenga Wodi ya mama na mtoto - Chemba
Wanawake wa Kata ya Songolo, katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamejitoa katika ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lililojengwa katika kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuchangia nguvukazi ili kupunguza changamoto za kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho Bw. Saidi Msigwa mbele ya timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya katika Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya mkoani Dodoma.
Amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa Kata ya Songolo walijitokeza katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ndicho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu cha kujengewa Wodi ya mama na Mtoto jambo lililopelekea wanawake wengi hasa wajawazito kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wialaya ya Kondoa.
Amesema kukamilika kwa Kituo cha afya cha Hamai kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya hasa vijiji vya jirani... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More