WANNE SIMBA WAITWA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE, YANGA ACHUKULIWA MMOJA TU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANNE SIMBA WAITWA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE, YANGA ACHUKULIWA MMOJA TU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NYOTA wanne wa Simba Queens wameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 27 timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kujiandaa na mchezo wa kufuzu Olimpiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwakani mjini Beijing, China.
Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo imewataja wachezaji hao ni Mwanahamis Omari Shurua ‘Gaucho’, Amina  Ally Bilal, Dotto Evarist Tossy na Amina Abdallah.
JKT Queens imeendelea kuwa timu yenye mchango mkubwa Twiga Stars baada ya kutoa wachezaji 12 ambao ni Fatuma Omar Jawadu, Najiath Abbas Idrissa, Maimuna Hamisi Kaimu, Fatuma Khatibu Salumu, Happyness Hezron Mwaipaja, Stumai Abdallah Athumani, Anastazia Antony Katunzi, Fatuma Bushir Makusanya, Zena Khamis Rashid, Donisia Daniel Minja, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Fatuma Mustapha Swalehe.

Alliance Queens ya Mwanza imetoa wachezaji watatu ambao ni Enekia Yona Kasonga, Aisha Khamis Masaka na Esther Mabanza Gind... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More