WANUFAIKA WA TASAF CHATO WAIBUKIA KWENYE UFUGAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANUFAIKA WA TASAF CHATO WAIBUKIA KWENYE UFUGAJI

Na Richard Bagolele - ChatoBaadhi ya wanufaika wa mpango wa TASAF awamu ya tatu Wilayani wameendelea kujiongezea kipato kwa kufuga aina mbalimbali za mifugo.Baadhi ya wanufaika wamesema kupitia ufugaji wameona ndio njia pekee ya kwao kujikwamua na hali ngumu ya maisha ambayo walikuwa nayo kabla ya kuingia kwenye mpango wa TASAF 3 wa kunusuru kaya masikini.Bi Sugwa Bushuwandama mkazi wa kijiji cha Mkungo kata ya Bukome Wilayani hapa anasema kupitia mpango wa TASAF 3 kwa kipato kidogo anachopata hivi sasa anao mbuzi 12 ambao mara kwa mara amekuwa anauza na kununua mahitaji mengine ya familia kama vile chakula.“mwezi uliopita niliuza mbuzi wawili nilienda kufanya manunuzi mnadani ambapo nilinunua gunia la mahindi la shilingi elfu 40 na nguo za wanangu” alisema Bi Sugwa huku akitabasamu.Kwa upande mwingine wanufaika hao wanasema kupitia miradi ya ufugaji wa Ng’ombe na mbuzi kwao imekuwa ni rahisi kutokana na urahisi pindi wanapotaka kuuza au kubadili kupata bidhaa nyingine kama vile ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More