WAOKAJI VITAFUNWA WAPEWA ELIMU YA KUJITANGAZA KWENYE MITANDAO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAOKAJI VITAFUNWA WAPEWA ELIMU YA KUJITANGAZA KWENYE MITANDAO

Na.Khadija seif,Globu ya jamii
*Washiriki wapewa fursa kushiriki mashindano ya keki juni 26
Tamasha la waokaji  kufanyika rasmi jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi ambao walijitokeza kwenye tamasha hilo Muandaaji Laura Mkula amesema imekua ni mara ya kwanza kuandaa shindano hilo na muitikio umekua mkubwa kiasi chake kuanzia mchakato wa fomu hadi kushiriki kikamilifu.
" Imekua ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo hasa waokaji wa vitafunwa kushindanishwa na kupata ujuzi mpya kuboresha biashara zao,"
Aidha,Mkula ametoa ushauri kwa washiriki wote kuboresha biashara zao huku swala la kujitangaza likipewa kipaumbele na kutengeneza mitandao ya kijamii Kama njia pekee ya kuwasiliana na wateja wao na kuwafikia kwa haraka zaidi.
"Mitandao ya kijamii ifanye biashara yako ya kwanza ili iweze kukupatia wateja wengi zaidi na kupika vitu mbali mbali kutokana na idadi ya wateja wako,"
Pia amepongeza washiriki wote ambao wameweza kujitokeza kwenye tamas... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More