Wasanii 8 wa Bongo Fleva watoka kapa tuzo za AFRIMMA 2018, Uganda na Kenya waiwakilisha vyema Afrika Mashariki - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wasanii 8 wa Bongo Fleva watoka kapa tuzo za AFRIMMA 2018, Uganda na Kenya waiwakilisha vyema Afrika Mashariki

Leo alfajiri kulikuwa na sherehe za utolewaji wa tuzo za AFRIMMA 2018 Mjini Dallas, Texas Marekani ambapo tumeshuhudia kwa mara nyingine Wasanii kutoka Tanzania wakishindwa kuchukua tuzo.


Khaligraph Jones

Tanzania ambayo ilikuwa inawakilishwa na wasanii kama Alikiba, Diamond Platnumz, Nandy, Vanessa Mdee, Ommy Dimpoz, Harmonize, Navy Kenzo na Jux wote wameshindwa kuchukua tuzo hizo za Afrimma 2018.


Afrika Mashariki waliotamba ni Khaligraph Jones kutoka Kenya ambaye ameshinda tuzo kwenye kipengele cha ‘Rap African Act’ huku Eddy Kenzo na Ykee Benda  kutoka Uganda wakichukua tuzo ya ‘Best Male East Africa’ na ya Msanii chipukizi.


Wengine walioshinda ni Fally Ipupa kakwara tuzo mbili ya Msanii bora wa mwaka na ile ya Leadership In Music.


Yemi Alade, Wizkid na Mr. Flavour hao wameshinda tuzo moja moja kwenye usiku huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki.


Licha ya kuwa Harmonize hajashinda tuzo, lakini alikuwa ni moja ya wasanii waliotumbuiza kwenye usiku huo wa uga... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More