Wasanii tunaingiza hela lazima tulipe kodi, tusiwaonee BASATA wanasimamia sheria – Barakah The Prince (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wasanii tunaingiza hela lazima tulipe kodi, tusiwaonee BASATA wanasimamia sheria – Barakah The Prince (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kuwa wasanii nchini waache kulalamika kuhusiana na malipo ya kibali cha kutoka nje wakati wanaenda kuperform kwani malipo hayo yanawasaidia BASATA kuweza kuendesha baadhi ya kazi zao ambazo zitaisaidia sanaa yetu.Barakah amesema ili sanaa yetu ikue ni lazima wasanii waende sawa na sheria ikiwemo kulipa kodi na kudai kuwa kulipia kibali hiyo ni sheria ambayo ipo karibia kila nchi ingawaje wasanii wengi walikuwa wamezoea janja janja kipindi cha nyuma.


Akikoleza hoja yake amesema kuwa kitendo cha kulipia ada BASATA zitawafanya wasanii waheshimike na kuwa na sauti ya kusikilizwa na kutatuliwa matatizo yao.


The post Wasanii tunaingiza hela lazima tulipe kodi, tusiwaonee BASATA wanasimamia sheria – Barakah The Prince (+video) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More