WASANII WAFURAHISHWA NA KUSIFU KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA YA UMEME (SGR) - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WASANII WAFURAHISHWA NA KUSIFU KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA YA UMEME (SGR)

Mataruma yakiwa tayari kwa ajili ya kupangwa kwenye tuta ili kutandika reli.MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza na wasanii mbalimbali, Wachezaji wa zamani na waandishi wa habari mara baada ya kufika katika kambi kubwa ya Soga mkoani Pwani wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea jinsi shughuli za ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme Starndard Gauge Railway (SGR) kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro unavyoendelea.
Wakiongeza katika ziara hiyo wasanii mbalimbali wamesifu juhudi za sreikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 kwa jinsi inavyotekelezwa na serikali kwa kasi kubwa na kuleta matumaini kwa watanzania.
Mradi huo unajengwa na kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchini Uturuki na kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 42 ambapo kazi mbalimbali zinaendelea kama vile kujenga madaraja, kupasua miamba ya milima kuunganisha tuta katika vipande mbalimbali, kutandika mataruma na reli na kus... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More