Wasanii Waguswa na Tuhuma Zinazomkabili Steve Nyerere. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wasanii Waguswa na Tuhuma Zinazomkabili Steve Nyerere.

Baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali katika tasnia ya filamu wameona kuwa jambo linaliendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu kumsema Steve Nyerere ni jambo baya na linamkosesha amani yeye na familia yake.


Lakini pia jambo hilo limemfanya Steve ukata tamaa na kupoteza tena ule moyo wa kujitolea kila linapotokea jambo, na ndipo walipoanza kufunguka na kuomba wamuache Steve kumuandama kwa tuhuma za kuwa anakula pesa za rambirambi kweny misiba.


Faiza Ally anasema , wasanii wa bongo movies wameshndea kuelewa umuhimu wa steve na ndio maana tangu tuhuma hizi zianze wamekuwa kimya bila kuongea chochote.Lakini pia yeye anamini kuwa Steve ni mtu muhimu sana katikati yao anaewaunganisha kwa moyo wake tena bila kulipwa wala kuombwa.


Faiza anasema kuwa watu wanasahau kuwa steve amewasaidia mambo mengi tofauti na misiba , amekuwa nao katika harusi, katikakazi na dili nyingi mbalimbali lakini leo hii wanasahau na kukaa wakicheka tu pale wanapoona msanii huyo anatuhumiwa vibaya.


Faiza anawaomba wasanii wote kusimama na kuungana pamoja ili kumtetea na kukanusha tetesi zinamzomkabili Steve Nyerere ili kuendelea kuweka heshima yake.Na kwa upande wa Aunty Ezekiel, anasema kuwa wasanii wamechagua kuzikwa na steve nyerere, hivyo waache kumbeza steve nyerere.


kila binadamu huwa anapewa  karama yakekatika hii dunia, tivu  hiyo ni karama yake.jamani tuacheni tumeamua wenyewe kuzikwa na tivu….I love you tivu akee.


Kwa upande wa soudy brown anasema kuwa pamoja na kwamba hapo awali jambo hili la steve llikuwa likichukuliwa kama utani lakini ifike  sehemu waavche kuendelea kufanya utani kwa sababu inamkatisha tamaa mhusika,kwa sababu katika familia yoyote kuna mtu mmoja huwa anatokea kwa ajili ya kuwaunganisha watu wote. 


 


The post Wasanii Waguswa na Tuhuma Zinazomkabili Steve Nyerere. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More