WASANII WAUNGANA KUMSAIDIA HAMIS ALIYEVIMBA MIGUU,WAISHUKURU SERIKALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WASANII WAUNGANA KUMSAIDIA HAMIS ALIYEVIMBA MIGUU,WAISHUKURU SERIKALI

WASANII wa fani mbalimbali nchini wameamua kumsaidia kijana Hamisi Salum anayesumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu kwa kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili ili apate matibabu kwani wanaamini atapona na kutimiza ndoto zake. 
Akizungumza jana Machi 12, 2019 kwa niaba ya wasanii wenzake, Msanii maarufu nchini Steve Nyerere amesema wanamatumaini makubwa Hamis atapona, kikubwa ni Watanzania kumuombea kwa Mungu. 
Amefafanua Hamis alishapelekwa nchini India kwa matibabu na kisha akarejea nyumbani Tanzania na baadae tena alipelekwa Muhimbili. 
Ameongeza wasanii katika kuhakikisha Hamis anapona na kutimiza ndoto zake wameamua kumfuata tena nyumbani kwao na kisha kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili akatibiwe. 
Steve Nyerere amesema baada ya wao kupaza sauti zao Rais Dk.John Magufuli amesikia na kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wameamua kumsaidia. 
"Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kujali wanyonge, wasanii tumepaza sauti zetu kuha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More