Washindi 15 wa promosheni ya ‘Tia kitu pata vituuz’ na DStv wapatikana - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Washindi 15 wa promosheni ya ‘Tia kitu pata vituuz’ na DStv wapatikana

Kampuni ya MultiChoice nchini kupitia king’amuzi chake cha DStv imechezesha droo yake ya tatu ya promosheni ya “Tia kitu, pata vituz” mapema leo katika makao makuu ya ofisi zake zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Thamani kwa wateja MultiChoice Tanzania Hilda Nakajumo akizungumza na waandishi wakati wa droo ya kupata washindi wa awamu ya 3 , kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Semvua na kushoto ni Afisa Uhusiano Grace Mgaya.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza washindi hao 15 wa awamu ya tatu, Mkuu wa kitengo cha Thamani kwa wateja MultiChoice Tanzania bi. Hilda Nakajumo alieleza kuwa, “Leo tumefanikiwa kupata washindi 15 washindi waliopatikana kutoka vifurushi vyote vya DStv kama Bomba, Family, Compact, Compact plus pamoja na Premium. Washindi hawa wanafanya jumla ya washindi wetu kufikia 45 tangu promosheni hii ilipoanza kutokea katika mikoa tofauti hapa nchini kama vile Mwanza, Kagera, Iringa pamoja na ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More