WASICHANA 10,000 WAFIKIWA NA TASISI YA MSICHANA INITIATIVE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WASICHANA 10,000 WAFIKIWA NA TASISI YA MSICHANA INITIATIVE

Na Humphrey Shao, Globu jamii
Zaidi ya Wasichana 10,000 wamefikiwa na huduma zitolewazo na tasisi ya Msichana Initiative katika kipindi cha miaka Miwili na nusu tangu kuanzishwa kwake nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo , Rebeca Gyumi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kongamano la Ajenda ya Msichana linalo Taraji kufanyika Agosti 11 mwaka hu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.
Gyumi amesema kuwa kupitia kongamano hilo jumla ya Washiriki 1000 watashiriki wakiwemo wasichana walio ndani ya shule na nje ya shule kutoka klabu za Msichana Café na Makundi ya watu wenye mahitaji maalum.
“kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwa tasisi hii tumeweza kuwafikia wasicha 10000 moja kwa moja hivyo katika mkutano wa mwaka huu 2018 tumekuja na kauli mbiu isemayo ‘Nafasi ya Jamii kwenye kuunda na kutetea haki za mtoto wa kike’ huku msisitizo mkubwa wa kauli hii mbiu ni kuangalia namna gani Wasichana... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More