WASOMI NCHINI WAASWA KUTUMIA ELIMU YAO VIZURI KUIKOMBOA JAMII - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WASOMI NCHINI WAASWA KUTUMIA ELIMU YAO VIZURI KUIKOMBOA JAMII

Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Wahitimu nchini wameaswa kutumia elimu yao vizuri katika kuwa chachu ya kuwakomboa wengine katika changamoto mbalimbali zinazowakabili ndani ya Jamii.
Hayo yalisemwa Jana na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake ccm mkoa wa Arusha, Yasmin Bachu wakati akizungumza katika mahafali ya 20 ya wanafunzi 154 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Enaboishu iliyopo mjini hapa.
Alisema kuwa, wanapaswa kutumia elimu hiyo waliyoipata kuwa watatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii kwani wao Ndio wanaotegemewa kuleta mabadiliko chanya.
Aidha aliwataka wanafunzi hao pia kuhakikisha wanatoa elimu na kupinga vitendo viovu vya madawa ya kulevya kwa vijana sambamba na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia ambao ndio umeshamiri katika jamii nyingi kutokana na mila na desturi zilizopo.
"nawaombeni jamani mkawe mfano wa kuigwa na muwe mabalozi wazuri wa kabadilisha Jamii Kwa kutoa elimu Kwa vijana wenzenu juu ya vitendo mbalimbali viovu, ili kupitia nyie tuweze kuona mabadi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More