Wataalam wa Afya Muhimbili Wanaendelea kuwajengea Uwezo Wataalam wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wataalam wa Afya Muhimbili Wanaendelea kuwajengea Uwezo Wataalam wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi


Wataalam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na wataalam wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili, endelea kufuatilia habari katika picha.
Daktari Bingwa wa macho kutoka Muhimbili Judith Mwende akimpima macho mgonjwa kwa kutumia mashine maalum ya kuangalizia Retina, kushoto ni Dkt. Mwita Machage wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine. 
Dokta Willybroad Massawe ambaye ni Dkt. wa upasuaji, pua, koo na masiko (kushoto) kwa kushirikiana na watalaam wengine wa MNH pamoja na wa hospitali ya Sokoine akimtoa mgonjwa matezi ya koo na matezi ya nyama ya pua (mafindofindo) upasuaji ambao huwa haufanyiki katika hospitali hiyo kutokana na ukosefu wa wataalam. 
Daktari Bingwa wa Patholojia kutoka MNH Innocent Mosha akifanya uchunguzi wa vivimbe ili kujua tatizo alilokuwanalo mgonjwa kwa ajili ya kuwasaidia Madaktari wa upasuaji k... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More