WATAALAM WANAWAJIBU WA KUINGIZA UTAALAM KATIKA UCHUMI WA VIWANDA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATAALAM WANAWAJIBU WA KUINGIZA UTAALAM KATIKA UCHUMI WA VIWANDA

Na Chalila Kibuda, Globu ya JamiiCHUO Kikuu Mzumbe kimesema watalaam katika sekta mbalimbali wanawajibu kuingiza uwezo wao katika uchumi wa viwanda ili kuendana na malengo ya serikali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi wakati wa kikao cha maafisa rasilimali watu kilichofanyika Chuoni hapo, amesema watalaam katika kada mbalimbali wanahitaji kutambua na kufungua fursa katika sekta ya viwanda katika kuhakikisha nchi inafikia malengo.
Amesema kuwa Chuo kimekuwa kikiendesha Program katika kada zinazozalishwa katika chuo ili kuhakikisha watalaam wanapeleka ujuzi wao ambao utasaidia taifa kuvuka mipango yake ya kufika kwenye uchumi wa viwanda vya ndani.
Profesa Ngowi amesema kuwa maafisa Rasilimali watu wanawajibu wa kuhakikisha kila anayefanya kazi katika viwanda anapanda kutokana na taratibu zilizowekwa ili kukidhi mahitaji ya wafanyakazi.
Kwa upande wa Mratibu wa Program hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Dkt Faisal Is... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More