Wataalamu Muhimbili Wawasili Musoma Kutoa Huduma za Afya - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wataalamu Muhimbili Wawasili Musoma Kutoa Huduma za Afya

Wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamewasili leo Musoma, mkoani Mara kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa hospitali za rufaa za mikoa nchini.

Lengo la ziara hii ni kuwaongezea ujuzi wataalamu wa hospitali za rufaa kupitia wataalamu wabobezi wa muhimbili ikiwa ni kutekeleza mpango mkakati wa MNH wa kuhakikisha inazitembelea hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ambao pengine wangepewa rufaa kwenda kupata huduma za kibingwa Muhimbili.

Baada ya timu ya wataalamu 14 kuwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma mkoani Mara, ilipokelewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Joachim Eyembe na hakusita kueleza furaha yake kwa ujio wa watalaamu hao wabobezi ambao watawajengea uwezo wataalamu wenzao katika maeneo ya upasuaji wa pua, koo, masikio na usingizi na kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wa... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More