WATAALAMU WA MANUNUZI YA UMMA WAASWA KUZINGATIA WEREDI KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATAALAMU WA MANUNUZI YA UMMA WAASWA KUZINGATIA WEREDI KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI

Na Woinde Shizza Globu ya jamii ,Arusha
Wataalamu wa manunuzi ya Umma nchini wametakiwa kuzingatia weredi katika utendaji wao wa kazi na kuepukana na vitendo vya ubadhirifu ,rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma, jambo litakalosaidia kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na kusaidia fedha hizo kutumika katika maendeleo mapana zaidi ya Taifa.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli,wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku tatu wa wataalamu na wabobezi wa manunuzi ya umma(IPPC) kutoka nchi 46 Duniani unaofanyika jijini Arusha,nchini Tanzania,Waziri wa fedha na mipango Dkt Mpango amesema mkutano huo unalenga kujadiliana namna ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia taknolojia mpya ya manunuzi .
‘’Ununuzi wa umma ndio sehemu kubwa ambapo fedha za bajeti zinapita, hivyo ukifanyika vibaya maana yake serikali inapata hasara ndio maana tunasisitiza weredi wa wataalamu wa manunuzi kwa sababu kuna mamunuzi hewa na miradi hewa ’amesema Dkt MpangoWaziri wa Fedha na Mip... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More