WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Elimu wahakikishe wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo ni wale waliovuka katika ngazi ya shule, kata, wilaya na mkoa, ambao wote ni wanafunzi halali wa shule na marufuku kuchezesha mamluki. 
“Endapo itabainika yupo mchezaji aliyeletwa kushiriki michezo hii ambaye si mwanafunzi (yaani mamluki) naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahusika kwa kuzingatia kanuni na sheria za mashindano haya,” amesisitiza.Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 9, 2018) wakati akifunguaMashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania yanayofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na wilaya zote nchini wahakikishe kuwa masomo ya haiba, michezo na stadi za kazi yanafundishwa kikamilifu kwenye shule zote za msingi. 
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema somo la elimu ya michezo kwa Shule za Sekondari nalo lifundishwe... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More