WATALAAM KUTOKA MUHIMBILI WAWASILI LINDI KUTOA HUDUMA ZA AFYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATALAAM KUTOKA MUHIMBILI WAWASILI LINDI KUTOA HUDUMA ZA AFYA

Madaktari Bingwa 11 pamoja na wataalam wengine wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) wamewasili katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa huo sanjari na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu amesema lengo la ujio wao katika hospitali hiyo ni kuwaongezea ujuzi watalaam wa hospitali za rufaa za mikoa nchini kupitia madaktari bingwa wa Muhimbili lakini pia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.

‘’Hospitali imeweka mkakati wa kuzitembelea hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo , lakini pia kama Muhimbili tunatekeleza agizo la serikali linaloelekeza kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibwa nje ya nchi hatua ambayo tayari MNH inaitekeleza hivyo utoaji wa huduma za fya kwa njia ya mkoba utasaidia kupunguza rufaa za wagonjwa ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More