WATALII WALAZAMIKA KUONGEZA SIKU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI KUSHUHUDIA TUKIO LA KUHAMA KWA MAKUNDI YA NYUMBU WAKITOKEA KENYA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATALII WALAZAMIKA KUONGEZA SIKU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI KUSHUHUDIA TUKIO LA KUHAMA KWA MAKUNDI YA NYUMBU WAKITOKEA KENYA.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Mkoani Mara,imeendelea kuwa maarufu Duniani na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia kwa ajili ya kujionea tukio la kila mwaka la kuhama kwa Makundi makubwa ya Nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya na kuingia Serengeti.

Tukio hili ambalo hutokea kuanzia mwezi Julai na wageni kulipa jina la “Great Wildebeest Migration” mwaka huu linatajwa kuvutia watalii wengi zaidi huku wengine wakilazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Serengeti wakingojea kushuhudia tukio hilo.Michuzi blog imeshuhudia Msururu wa Magari ya kubeba watalii yakiwa na wageni kando ya Mto Mara kusubiri kujionea hali inavyokuwa wakati wanyama hao wakivuka kwa makundi kutoka upande mmoja wa mo kuingia Hifadhi ya Serengeti.

Eneo la Mto Mara ambapo Wanyama hawa wamekuwa wakivuka linatajwa kuwa na Vivuko 10 hali inayochangia waongoza watalii kufuata mwenendo wa Nyumbu kwa ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More