WATANZANIA MNAOSOMA CHINA JITUMENI KWA AJILI YA MAENDEO YA TAIFA-BALOZI KAIRUKI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATANZANIA MNAOSOMA CHINA JITUMENI KWA AJILI YA MAENDEO YA TAIFA-BALOZI KAIRUKI.

 WATANZANIA wanaosoma nchini China wametakiwa kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu,kujituma na kujitolea kwa manufaa ya taifa la Tanzania ikiwemo kuchangamkia fursa za maendeleo.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania nchini humo (TASAFIC) Desemba mosi mwaka huu.Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Watanzania wanaosoma China na Ubalozi wa Tanzania, ulilenga kuleta pamoja watanzania wanaosoma miji mbalimbali kama Dalian, Najing na Tianjing.

Alisema watanzania wanaoishi nchini humo wanapaswa kuangalia fursa za maendeleo kuwa wabunifu kujituma na kujitolea kwa manufaa ya taifa la Tanzania.“Ili Tanzania inufaike na mafanikio ya China Kiuchumi ni lazima kuwe na wataalamu wenye ujuzi na maarifa inayokwenda sambamba na teknolojia ya kisasa,”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawakala wa elimu ya vyuo vikuu nje ya nchi, Global Education Link, Abdul Malik Mollel ameipongeza... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More