WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA SEPT 15, 2018 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA SEPT 15, 2018

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.Tanzania itashiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi tarehe 15 Septemba, 2018. Tukio hili litafanyika chini ya kauli mbiu ya “Let’s Do It”.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah amewaomba Watanzania kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini na kujumuika na watu zaidi ya milioni 20 katika nchi 150 duniani kusherekea Siku ya Usafi Duniani ya kwanza kwa kusafisha maeneo mbalimbali ya umma hususani fukwe, njia za maji na mito.
Alisema usafi utafanyika katika maeneo 70 kwenye mikoa 16 hapa nchini ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mwanza, Mtwara, Simiyu, Mbeya, Shinyanga na baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar.
Usafi utafanyika katika maeneo 33 yaliyopo katika manispaa zote za jiji la Dar es salaam na maeneo 37 yatafanyiwa usafi katika mikoa mingine. Baadhi ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More