WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA SEPT 15, 2018 - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA SEPT 15, 2018

 Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah (Katikati) akiwaomba Watanzania kujitokeza siku ya mazingira duniani September 15, 2018 katika maeneo yapatayo 33 ya Tanzania. Pembeni ni waratibu wa Nipe Fagio, Catherine Nchimbi (kulia) na Navonaeli Kaniki (kushoto). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Tanzania itashiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi tarehe 15 Septemba, 2018. Tukio hili litafanyika chini ya kauli mbiu ya “Let’s Do It”.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah amewaomba Watanzania kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini na kujumuika na watu zaidi ya milioni 20 katika nchi 150 duniani kusherekea Siku ya Usafi Duniani ya kwanza kwa kusafisha maeneo mbalimbali ya umma hususani fukwe, njia za maji na mito.
Alisema usafi utafany... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More