WATANZANIA WATAKIWA KUENZI VITU VYA KIASILI KUVUTIA WATALII - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATANZANIA WATAKIWA KUENZI VITU VYA KIASILI KUVUTIA WATALII

Na Zainab Nyamka, Globu ya JamiiWATANZANIA wameombwa kuenzi vitu vya asili ili kudumisha utamaduni na kuvutia watalii wengi kuja nchini.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga alipokua anazungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Nchini baada ya kuwatembelea ofisini Kwao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri amesema kuwa moja ya vitu ambayo watanzania wanatakiwa kuvidumisha ni utalii wetu ili kuweza kuongeza pato la Taifa.
Amesema, kwenye baadhi ya sehemu ambazo zimesahaulika ni Utalii wa Utamaduni kitu kinachopelekea kupotea kwa tamaduni zetu ikiwemo vyakula, mavazi, sanaa za mkono na michoro, michezo pamoja na lugha ya Kiswahili.
Amesema, kuanzia mwaka huu wameweka mwezi Septemba kuwa mwezi wa Utamaduni utakaokuwa unajulikana kama Urithi Festival ambapo kutakuwa na maonesho mbalimbali ya vitu vya utamaduni ili kuvutia watu wa nje waje kujionea namna utamaduni wa watanzania ulivyo.

Hasunga amesema kuwa, lengo kuu la maonesho hayo ni kuongeza wata... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More