watanzania watakiwa kununua bidhaa za kwenye maduka yanayotambulika - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

watanzania watakiwa kununua bidhaa za kwenye maduka yanayotambulika

WATANZANIA wameshauriwa kununua bidhaa kwenye maduka yanayotambulika na kuacha kuamini matapeli wanaotumia nembo za kampuni kubwa kuwahadaa.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Kampuni ya Elite Computers yenye dhamana ya kusambaza bidhaa za Apple hapa nchini, wakati wa hafla ya kutambulisha simu mpya ya iPhone XR.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Aqil Kurji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Elite Computers alisema pamoja na kwamba Apple inaaminika kwa kuzalisha bidhaa bora lakini kumekuwa na wajanja wachache ambao wamekuwa wakitumia nembo ya kampuni hiyo kwa kuwauzia watanzania bidhaa zisizo na ubora.
“Leo Elite Computers ambao ni wakala rasmi wa Apple nchini tumetambulisha simu mpya ya iPhone XR  ambayo tunaamini kuwa itaendana na mazingira ya Kitanzania kwa asilimia 100 kutokana na kuzingatia hali halisi.
“Sifa kuu ya simu hii kwanza inadumu na chaji kwa saa 25 hadi 65 pia ina usalama kwani mteja atatumia uso wake kama paswedi(Face Id) na hivyo itarahisisha masu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More