WATEJA DSTV KUSHUHUDIA LIGI KUBWA ULIMWENGUNI KWA GHARAMA NAFUU,ZIPO ZA UINGEREZA,HISPANIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATEJA DSTV KUSHUHUDIA LIGI KUBWA ULIMWENGUNI KWA GHARAMA NAFUU,ZIPO ZA UINGEREZA,HISPANIA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WATEJA wa DStv wanatarajia kuanza tena kushuhudia moja ya ligi maarufu kabisa duniani ikiwemo Ligi ya Italia– Serie A.
Hatua hiyo inakuja baada ya MultiChoice kutangaza leo jijini Dar es Salaam kuwa kuanzia msimu huu, ligi hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.Mbali na Serie A ambapo atakuwepo nguli wa soka Cristiano Ronaldo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia ligi na michuano mikubwa mingi duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza (Premier League) na La Liga.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema mbali na habari za kurudi kwa Serie A, DStv pia itaongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu.Amesema watumiaji wa DStv Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 100 katika michuano ya Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.
Ameongeza kuwa watumiaji wa kifurushi cha DStv ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More