Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG)

Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa. 
Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 
“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mba... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More