WATEJA WA ZAMANI DAWASA WAANZA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJI KUPITIA KAMPENI YA TUNAWAHITAJJ - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATEJA WA ZAMANI DAWASA WAANZA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJI KUPITIA KAMPENI YA TUNAWAHITAJJ

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea kuwapokea na kuwarudisha huduma ya maji kwa wateja waliokatiwa huduma hiyo kutokana na kushindwa kulipa bili zao.
Hatua hiyo imekuja baada ya DAWASA kuanzisha kampeni mpya ya Tunawahitaji inayowataka wateja wote wa zamani kurudishiwa huduma za maji na wakubaliane watalipa katika mfumo gani.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni ya 'Tunawahitaji' lengo kuu ni kuona wateja wote takribani 10000 waliokatiwa maji wanaanza kupata tena huduma hiyo.
Luhemeja alisema kuwa amewaagiza maafisa wote wa utawala wafanye hivyo haraka,lengo la Tunawahitaji ni kuwatafuta wateja wa zamani na wapya ili waunganishiwe maji na hiyo ni kampenibya kudumu.Kampeni hiyo itawahusisha wateja wote waliokatiwa huduma ya maji na kupitia kwa mameneja wa mikoa yote ya DAWASA kwa pamoja wakubaliane watalipa kwa miezi mingapi madeni ambayo wanadaiwa.
Kwa upande ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More