Watendaji lazima wawajibike katika ukusanyaji wa kodi -Kaimu Mkurugenzi Temeke - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watendaji lazima wawajibike katika ukusanyaji wa kodi -Kaimu Mkurugenzi Temeke

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imesema kuwa katika kupata maendeleo ya nchi lazima Watendaji wawajibike katika ukusanyaji wa mapato.
Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Rugambwa Banyikila wakati mafunzo kazi kwa Watendaji Kata na Mitaa yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato nchini Mkoa wa Temeke kwa ajili ya uhakiki wa nyumba kwa Mkoa huo.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano katika miradi inayotekeleza asilimia kubwa inatokana na hivyo hakuna sababu ya kumuangusha Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Banyikila amesema Watendaji wa Kata na Mitaa wametakiwa kuorodhesha nyumba ili kuweka takwimu na kurahisisha katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na nyumba hizo.
Amesema TRA iko imara hivyo Manispaa itatoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki nyumba kurahisisha ukusanyaji wa kodi ya majengo.
Nae Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke Gamaliel Mafie amesema kuwa maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa watarahisha katika ukusanyaji kodi ya majengo kutokana na... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More