WATENDAJI SIMAMIENI SHERIA ILI KUTATUA UTOROSHAJI WA RASILIMALI ZA MIFUNGO - ULEGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATENDAJI SIMAMIENI SHERIA ILI KUTATUA UTOROSHAJI WA RASILIMALI ZA MIFUNGO - ULEGA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega,amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na Mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mhe.Ulega Amefungua Mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5 kila mwaka na hufanyika  Dodoma na hujumuisha Ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa Asili.
Mhe.Ulega amesema kuwa lengo kuu la Mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.
Aidha amesema kuwa zoezi hili linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.
Mhe.Ulega amesesisitaza kuwa Sekta ya Mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishwa katika mpango kabambe wa Mifug... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More