Watoa Huduma NHIF watakiwa kuacha udanganyifu- Gambo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watoa Huduma NHIF watakiwa kuacha udanganyifu- Gambo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akifungua Mkutano wa Wadau wa NHIF, Mkoa wa Arusha.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SERIKALI imewataka Watoa Huduma waliosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuachana na udanganyifu katika utoaji wa huduma kwa wanachama wake kwa kuwa jambo hilo ni kurudisha nyuma maendeleo ya Mfuko ambao ni nguzo kubwa katika utoaji wa huduma za matibabu.
Akifungua kikao cha Wadau wa NHIF, Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo amesema kuwa udanganyifu katika huduma ni adui mkubwa wa uimarishaji wa chombo hicho ambacho kwa sasa kinahudumia wananchi wengi na wanaohitaji huduma ambazo gharama zake ni kubwa.
“Niwaombe sana wadau wote hususan wanachama wa Mfuko, ni vyema kila mmoja kwenye nafasi yake akawa mlinzi wa huduma anazopata ili Mfuko huu uwe imara zaidi na uendelee kuhudumia wananchi, mimi binafsi nikiri tu kwamba bila ya kuwa na kadi ya NHIF nisingeweza kumudu gharama za matibabu, nimemuuguza Mama yangu na alihitaji matibabu yenye gharama kubwa lakini kwa ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More