WATU 20 MIKONONI KWA POLISI TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI...WAZIRI LUGOLA AELEZA KINACHOENDELEA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATU 20 MIKONONI KWA POLISI TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI...WAZIRI LUGOLA AELEZA KINACHOENDELEA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WaZIRI wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi hadi sasa linawashikilia watu 20 kwa ajili ya kuwahoji na kuchukua ushahidi utakaowezesha kupatikana kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na vyombo vya habari kuhusu matukio mbalimbali yakiwamo ya utekaji watu.
Waziri Lugola amesema kwamba Jeshi la Polisi nchini wanaendelea  kumtafuta Mo Dewji na kuwasaka walimtoka.
"Watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na kutoa taarifa ambazo zitasaidia kupata ushahidi ambao utasaidia kumpata Mo Dewji," amesema Waziri Lugola.Pia amesema pamoja na kushikiliwa kwa watu hao kwa ajili ya ushahidi wa kufanikisha kupatikana kwa Mo na kwamba watakaohojiwa na ikibainika wanastahili kuachiwa basi iwe hivyo ndani ya saa 24.
"Nimetoa maagizo kwa Polisi kuhakikisha walioshikiliwa wanahojiwa na ndani ya saa 24  kama hakuna sababu ya kuendelea kushikiliwa waachiwe," amesema.Alipoulizwa sababu za... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More