WATU 20 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA UCHUNGUZI ZAIDI JUU YA KUTEKWA KWA MO DEWJI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATU 20 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA UCHUNGUZI ZAIDI JUU YA KUTEKWA KWA MO DEWJI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kwamba watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini hadi sasa kwa ajili ya uchunguzi juu ya kutekwa kwa Mfanyabiashara Bilionea, Mohammed ‘Mo’ Dewji juzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Lugoma amesema kwamba Jeshi la Polisi nchini linaendelea kumtafuta mfayabiashara huyo likiwa na imani kubwa ya kumpata akiwa salama.
Waziri Lugola amelitaka jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wake ili lisiwashikilie washukiwa kwa zaidi ya saa 24.
Aidha, Waziri Lugola amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazoweza kulisaidia Jeshi la Polisi kupatikana kwa Mohammed Dewji.

Watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi juu ya kutekwa kwa Mfanyabiashara Mohammed ‘Mo’ Dewji 

“Sababu za matukio ya kutekwa yanayotokea ni pamoja na kisiasa, kiuchumi, kimapenzi na njaa ili mtu apate fedha na sababu za kutekwa kwa Mohamed Dewji zitajulika hapo wahalifu watakapojulikana,” amesema Lugola.... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More