WATU 300 DAR WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MACHO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATU 300 DAR WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MACHO

*Ni baada ya Hospitali ya macho ya Dk Agarwal kuamua kufanya uchunguzi bila malipoNa Said Mwishehe,Globu ya jamiiWATU zaidi ya 300 wamefanyiwa uchunguzi wa macho yao na matatizo mbalimbali yamegunduliwa ambayo husababisha uoni hafifu au upofu huku pia ukitolewa ushauri wa namna ya kutunza macho.
Hivyo kati ya hayo yaliyogundulika, yamejumuisha magonjwa ya mtoto wa jicho, mzio wa macho, matatizo ya kisukari yalioathiri macho, presha ya macho na mengine. Uchunguzi huo umefanywa na Hospitali ya macho ya Dk Agarwal ambayo imeamua kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa waliobainika kuwa na matatizo ya macho, hasa kwa wale wagonjwa wenye mtoto wa jicho bila tozo yoyote.Uamuzi huo ni kama mchango wake katika jamii katika harakati za kupunguza na kuondoa mzigo wa upofu hapa nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa na Mshauri wa magonjwa ya macho na upasuaji wa Retina katika hospitali hiyo Dk. Emeritus Chibuga. Amefafanua kuwa Hospitali ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More