Watu 40 waripotiwa kufariki dunia katika shambulio lililotokea kwenye misikiti miwili nchini New Zealand - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watu 40 waripotiwa kufariki dunia katika shambulio lililotokea kwenye misikiti miwili nchini New Zealand

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Waziri Mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo lililotanda ‘kiza kikubwa’ siku ya leo nchini humo.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, kamishna wa polisi Mike Bush amesema, lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa “gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia”.

Walioshuhudia mkasa huo wameambia vyombo vya habari kwamba walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini wanaovuja damu nje ya mskiti wa Al Noor.

P... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More