Watu 63 wafariki katika harusini Afghanistan. - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watu 63 wafariki katika harusini Afghanistan.

Watu wapatao 63 wameuawa na wengine 182 wamejeruhiwa katika mripuko wa shambulio la bomu la kujitoa muhanga, uliotokea katika sherehe ya harusi hapo jana katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.


Shambulio hilo limetokea huku kundi la Taliban pamoja na Serikali ya Marekani, wakiwa wanajaribu kujadili makubaliano ya Marekani kuondoa vikosi vyake vya kijeshi nchini Afghanistan, ili kundi la Taliban lifanye mazungumzo ya kutafuta amani na Serikali ya Afghanistan ambayo inaungwa mkono na Marekani. Kundi la Taliban limekataa kuhusika na shambulio hilo na limelilaani.


Shambulio hilo limetokea magharibi mwa mji wa Kabul kwenye idadi ndogo ya Washia, katika ukumbi wa harusi uliokuwa umejaa watu waliokuwa wakisherehekea harusi hiyo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Nasrat Rahimi, amesema leo kwamba miongoni mwa waathirika ni wanawake na watoto.


 Tweet... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More