Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wameogopa ushindi wa kisulisuli – Polepole - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wameogopa ushindi wa kisulisuli – Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa watu wa vyama vya upinzani ni waungwana sana kwakuwa wameamua kujitoa wenyewe kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, baada ya kukiona chama hicho kilivyo imara na hawawezi kushindana nacho.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole


Polepole amesema hayo leo Novemba 13, 2019, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.


“Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wametazama wakasema mambo yatakayotokea kwenye uchaguzi huu si ya mchezo, kwetu sisi ile 2014 inawezekana ulikuwa ushindi wa Tsunami ila wa mwaka huu utakuwa ni ushindi wa kisulisuli na ndiyo maana wakaamua kabla hatujafika pabaya wakaweka mpira kwapani”, amesema Polepole.


Aidha Polepole amevitaka vyama vya upinzani kujifunza kulingana na historia iliyopita kwakuwa kuna baadhi ya maeneo hawana wafuasi kabisa kama ilivyo CCM.


“Wanasema historia ni somo la kale la sasa na li... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More