Watu wenye Ulemavu waiomba Tume ya Uchaguzi kuwawekea Mazingira Rafiki - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watu wenye Ulemavu waiomba Tume ya Uchaguzi kuwawekea Mazingira Rafiki

Mbarouk Salim ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Taifa akizungumza na na Watu wenye ulemavu (hawapopichani)

Na.Vero Ignatus,Arusha.
Watu wenye Ulemavu mkoa wa Arusha wameiomba Tume ya uchaguzi kuweka mazingira rafiki kwao ili waweze kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa daftrari la wapiga kura na kutimiza haki yao ya kikatiba bila kupata vikwazo vinavyotokana na hali zao.

Yunisi Urassa ni Katibu wa Shirikisho la vyama vya Walemavu wilaya ya Arusha ametoa maombi hayo huku akisisitiza kuwepo kwa mazingira rafiki katika vituo vya kujiandikisha ili viweze kufikika kwa urahisi na watu wote katika kikao cha Tume ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa,wawakilishi wa makundi maalumu katika jamii.
Mbarouk Salim ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Taifa amesema kuwa zoezi hilo litaanza hivi karibuni na tayari ziko asasi za kiraia zilizopewa kibali cha kutoa elimu za raia kwa wapiga kura ili waweze kutumia haki yao ya kikatiba.
Wajumbe kutoka ka... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More