WATUMISHI WA TUME WANAOSHIRIKI KATIKA UKAGUZI WA RASILIMALI WATU KWA TAASISI 56 WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WATUMISHI WA TUME WANAOSHIRIKI KATIKA UKAGUZI WA RASILIMALI WATU KWA TAASISI 56 WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI

Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wanaoshiriki katika Ukaguzi wa Rasilimali watu  katika Mikoa mitano yenye jumla ya Taasisi 56 zilizopo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la  kuangalia kiwango cha uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika usimamizi na uendeshaji wa Rasilimali watu katika Utumishi wa Umma wametakiwa kuzingatia maadili.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma,   Richard Odongo amezungumza na watumishi wa Tume pamoja na maafisa wanaofanya ukaguzi huo jijini Dar es Salaam na amewaasa kuzingatia maadili na wahakikishe wanatekeleza jukumu hili kwa uadilifu na uaminifu  mkubwa.
Odongo amesema kuwa Watumishi wa Tume wanaokwenda kufanya ukaguzi huo wanapaswa watambue kuwa wamebeba dhamana kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma hivyo wakati wote wajiepushe na mienendo isiyofaa, wakatekeleze jukumu hili la kisheria la ukaguzi wa rasilimali watu kwa weledi, wazingatie maadili na wahakikishe wanatoa maamuzi ya haki na taarifa sahihi na kwa wakati.
Mikoa itak... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More