Watumishi wa Umma Kuweni na Subira Ongezeko la Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Watumishi wa Umma Kuweni na Subira Ongezeko la Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa


Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa, amewataka watumishi wa umma kuwa na subira kwa sababu Serikali inaendelea na mchakato wa kuwatambua watumishi wa umma halali na kufanya ulinganifu wa mishahara katika kada mbalimbali ili watumishi hao waanze kulipwa mishahara stahiki. 
Waziri Mkuu Majaliwa ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe Pascal Haonga, lililohoji juu ya ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma.
Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa mwanzoni nchi ilikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakilipwa mishahara na posho mbalimbali hivyo, ili kuwatambua watumishi halali Serikali iliamua kufanya uchunguzi na kuwagundua watumishi hao hewa.
Pia, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine wa kuwatambua watumishi wenye vyeti stahiki vya kufanya kazi mbalimbali Serikalini kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.
Mhe. Ma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More