WAVAMIZI SHAMBA LA MITI BIHARAMULO WAPEWA MIEZI 3 - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAVAMIZI SHAMBA LA MITI BIHARAMULO WAPEWA MIEZI 3

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati)  akizungumza   na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe.  Mtemi Simeoni (kushoto)   wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa  ukubwa  wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita., Kulia ni Meneja wa shamba hilo, Edward Nyondo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu.
Ametoa muda huo ili wananchi waliolima mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na pamba waweze kuvuna mazao yao kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More