WAWEKEZAJI RANCHI ZA TAIFA WATAKIWA KUSAINI MIKATABA MIPYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAWEKEZAJI RANCHI ZA TAIFA WATAKIWA KUSAINI MIKATABA MIPYA

Na Avila Kakingo, Globu ya JamiiWAWEKEZAJI wa vitalu vya ufugaji katika ranchi ya taifa watakiwa kusaini mikataba mipya kwaajili ya kuendelea na ufugaji wa kibiashara katika ranchi za taifa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura wakati wa kusaini mikataba mipya ya uwekezaji katika lanchi ya taifa jijini Dar es Salaam leo.
Wambura amesema kuwa mikataba hiyo mipya itaanza kutumika mara moja hivyo mwekezaji ambaye atakuwa hajasaini mkataba  mpya atahesabika kuwa hana nia tena ya kuendelea na uwekezaji kaika ranchi za taifa.
"Mikataba mipya itaanza kutumika mara moja hivyo mwekezaji ambaye atakuwa hajasaini mkataba  huu mpya atahesabika kuwa hana nia tena ya kuendelea na uwekezaji katika ranchi za taifa na hivyo ataondolewa". amesema Wambura
Amesema kuwa utaratibu wa kuwaondoa wawekezaji ambao hawana mikataba mipya katika ranchi za taifa utaanza kutekelezwa mara moja.
 Kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) iliingia mkataba na wawek... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More