Wawili wakamatwa, mmoja afutiwa mkataba ujenzi wa hospitali ya Wilaya - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wawili wakamatwa, mmoja afutiwa mkataba ujenzi wa hospitali ya Wilaya

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kusitisha mkataba na fundi anayehusika na ujenzi wa jengo la maabara katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kalambo huku akimtaka Mkurugenzi huyo kutafuta chumba katika eneo hilo ili asimamie kwa karibu ujenzi unaoendelea na kuhakikisha unaisha kwa wakati.
Ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo hivi karibuni baada ya kuitaka mikoa yote kusimamia ujenzi wa hospitali za wilaya na kufikia tarehe 13 hadi 25 Mei, 2019 majengo yote yawe yameshapauliwa na mikoa hiyo kutuma picha za majengo saba ya hospitali hizo.
Kwa kutekeleza hayo Wangabo amewaagiza mafundi wote wanaosimamia ujenzi wa majengo hayo saba kuhakikisha wanafikia usawa wa linta ifikapo tarehe 10 mwezi Mei mwaka huu na hatimae kumalizika kwa wakati.
Wangabo ameyasema hayo alipotembelea eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo na kuk... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More