WAWILI WONGEZWA KESI YA KITILYA, WAACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA. WASOMEWA MASHTAKA MAPYA 58 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAWILI WONGEZWA KESI YA KITILYA, WAACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA. WASOMEWA MASHTAKA MAPYA 58

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea mashtaka mapya 58 yakiwemo ya utakatishaji  fedha na kuisababishia serikali hasara ya dola milioni sita aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake wawili ambao ni, aliyekuwa Miss Tanzania 1999 Shose Sinare na Sioi Solomon baada ya mapema leo asubuhi kuwafutiwa mashtaka nane yaliyokuwa yanawakabili.

Hata hivyo katika mashtaka mapya TAKUKURU imewaongeza watuhumiwa wawili kwenye kesi hiyo ambao ni  Bedason Shallanda  ambaye ni Kamishina wa  uchambuzi wa  madeni kutoka Wizara ya Fedha  na msaidizi wake Alfredy  Misana.

Katika kesi hiyo mpya washtakiwa wanakabiliwa na  na mashtaka matatu ya kughushi, mashtaka mawili ya kutoa nyaraka za uongo, shatka moja la kujipatia pesa takribani dola milioni mia sita kwa njia za udanganyifu shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya fedha, shtaka moja la kuongoza uhalifu, mashtaka 49 ya  utakatishaji... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More