WAZAZI WATAKIWA KUONDOKANA NA DHANA POTOFU. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZAZI WATAKIWA KUONDOKANA NA DHANA POTOFU.


Na Frankius Cleophace Tarime.

Wazazi na walezi Wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kuondokana na dhama potofu kwa kupotosha jamii pale seriklai inapopeleka huduma ya afya huku wakitakiwa kukujenga tabia za kupima afya zao mara kwa mara bila kusahua watoto wa kike ili kuondona na vifo vya ghafla ambavyo vimekuwa vikijitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara Mchungaji Abel Obura kipindi akifunga tamasha la kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ukiwemo Ukeketaji lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY nakufanyika katika Shule ya Msingi Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Mchungaji amesema kuwa jamii imekuwa ikipotoshwa pale serikali inapopeleka madawa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya za watoto nakusababisha baadhi ya watoto wengine kokosa huduma hiyo.“Serikali inaleta dawa za minyoo lakini jamii inapotoshwa kuwa wakimeza dawa hizo hawatazaa jambo ambalo siyo kweli na serikali inaleta dawa ambazo tayari zimethibitishwa hivyo sasa jamii iondokane na dhana potofu” alisema Mchungaji.

Pia Mchungjai amewataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwapima watoto wao kwani ni haki zao za msingi ikiwemo kupatiwa pia elimu ya msingi mpaka sekondari.

Kwa upande wake Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la RIGH TO PLAY ambao wanatoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia kupitia matamasha ambayo yanahusisha michezo mbalimbali yakiwemo maigizo, Nyimbo, Ngoma, Mpira wa miguu kwa wasichana, kuvuta kamba na Mashariri, michezo hiyo imebeba ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia.

“Michezo inakusanya watu wengi hivyo sisi kama shirika tumeamua kutumia michezo kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa katika jamii ya Mkoa wa Mara ili kulinda na kutetea haki za watoto ikiwemo kupata elimu” alisema Leah.

Aidha wananchi na wakazi wa kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti mkoni Mara wanazidi kupongeza uwepo wa matamasha hayo ya kutoa elimu katika jamii huku wasema kuwa suala la ukeketaji linazidi kupungua kila kukicha bali elimu ienndelee kutolewa katika jamii ili kuondoa usiri uliopo kwa sasa.

“Baada ya serikali kutilia mkazo suala la kupinga ukeketaji kuna usiri mkubwa unafanyia sasa elimi izidi kutolewa katika maeneo ya vijijini” walisema Wananachi hao.
Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkiani Mara Mchungaji Abel Obura akifunga tamasha hilo la kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji lililoandaliwa na shirika la RIGTH TO PLAY.
Leah Kimaroambaye ni mwezeshaji kutika Shirika la RIGHT TO PLAY akitoa Elimu ya kupinga Ukatili katika jamii kwenye tamamsha liloandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Maburi kata ya Nyambureti wilayani Serengeti Mkoani Mara.
mgeni rasmi ambaye ni Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara, Mchungaji Abel Obura akisalimiana na wachezaji baina ya timu ya Nyambureti Sekondari FC na Kerukerege FC. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>


Source: Issa MichuziRead More