WAZAZI, WATOTO OMBAOMBA KUSHTAKIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZAZI, WATOTO OMBAOMBA KUSHTAKIWANa Fatma Salum – MAELEZOSERIKALI imewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwakamata na kuwashitaki mahakamani watoto pamoja na wazazi wao ambao huzagaa mitaani kuombaomba.
Agizo hilo limetolewa leo bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza, lililohoji ni lini Serikali itachukua hatua ya kuwaondoa ombaomba Jijini Dar es Salaam.
Kakunda alibainisha kuwa ni kweli ombaomba wengi zaidi wapo Jijini Dar es Salaam kutokana na kuwepo kwa vivutio vingi ikiwemo watu wenye imani mbalimbali ambao wengine huwapatia fedha ombaomba hao kama sehemu ya ibada.
“Kuzagaa kwa ombaomba kimekuwa chanzo kimojawapo cha uchafuzi wa mazingira na mara kadhaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imechukua hatua mbalimbali za kuwaondoa ikiwemo kuwakamata na kuwarudisha kwao lakini wamekuwa wakirudi,” alisema Kakunda.
Alieleza kuwa mwaka 2013 ombaomba wapa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More