Waziri akusanya sh mil 280 akizindua mashindano ya mbio za baiskeli kusaidia sekta ya elimu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri akusanya sh mil 280 akizindua mashindano ya mbio za baiskeli kusaidia sekta ya elimu

NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda amezindua mpango wa mashindano ya mbio za baiskeli na kufanikisha kukusanya Sh milioni 280 kati ya Sh milioni 340 zinazotarajiwa kukusanywa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la 'Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge', yameandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini nchini -Acacia kwa kushirikiana na Tasisi binafsi kutoka nchini Canada - CanEducate.

Akizungumza katika uzinduzi wa uchangiaji wa mashindano juzi jijini Dar es Salaam, Kakunda alitoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuchangia mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 3, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kakunda ambaye alimwakilisha Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alisema malengo ya mashindano hayo yanaenda sambamba na malengo ya serikali katika kurahisisha mazingira ya utoaji elimu nchini. "Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani na kufuta a... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More