WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI

Na. Vero Ignatus, Arusha

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amelazimika kusitisha ziara kwa masaa mawili na nusu akisubiri kisima katika kijiji cha Levolosi Kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru kinachochimbwa kitoe maji kabla ya kwenda kusaini mkataba.

Aidha Prof. Makame Mbarawa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumrudisha Wizarani mara moja Mhandisi wa Miamba Amir Msangi kwa uzembe wa kutoonekana kwenye eneo la mradi.

Waziri alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea Kijiji cha Levolosi, Kata ya Kimnyaki kujionea zoezi la uchimbaji wa visima vitatu na baada ya hapo alitia saini ya mkataba wa ujenzi wa mtandao mpya wa maji,mitambo ya kutibu maji safi ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA na ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA Kanda ya Kati wenye thamani ya Sh.bilioni 520.

Prof.Mbarawa alisema serikali imeamua kuleta wataalam wake toka Wizarani ili wasimamie na kujifunza Teknolojia mpya ya uchimbaji visima vikubwa kwa ajili ya kuweza kufundiaha wenzao utaalam huo hapo ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More